Nyika awaita mashabiki uwanja wa Taifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2018
Nyika awaita mashabiki uwanja wa Taifa
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika amewataka mashabiki wa mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania wajitokeze kwa wingi kesho uwanja wa Taifa kuipa sapoti timu yao itakapokuwa inachuana na USM Alger kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mchezo huo wa kukamilisha ratiba kwa upande wa Yanga utapigwa kuanzia saa moja jioni.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Nyika amesema wamedhamiria kushinda mchezo huo.

Katika hatua nyingine, Nyika amesema Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji atakuwepo uwanja wa Taifa kuushuhudia mchezo huo.

Nyika amesema jana walikuwa na kikao na Manji na aliwahakikishia kuwa atakuwa sehemu ya uongozi wa Yanga utakaokuwepo uwanja wa Taifa.

Leo Mwenyekiti huyo atajumuika na wachezaji pamoja na viongozi wengine wa Yanga kupata chakula cha jioni.

Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam leo tayari kwa mchezo huo wa kesho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’