Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji atakuwepo kwenye uwanja wa Taifa keshokutwa Jumapili kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya USM Alger.
Manji aliyekuwa kimya kwa muda mrefu imeelezwa tayari amerejea rasmi kwenye nafasi yake.
Wakati huo huo uongozi wa Yanga umesema mgeni rasmi kwenye mchezo huo atakuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa keshokutwa ili kuipa sapoti timu.
Lakini pia mchezo huo utatumika kuwapa fursa wakazi wa mkoa wa Dar es salaam kumuaga mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye amestaafu na sasa akiwa na majukumu ya Umeneja wa Yanga.
Viingilio vya mchezo huo;
VIP A - Tsh 10,000/-
VIP B na C - Tsh 7,000/-
Mzunguuko - 3,000/-

ADVERTISE HERE