USM Alger yawasili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Aug 2018
USM Alger yawasili
Kikosi cha USM Alger kimewasili nchini jana saa moja jioni tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Wenyeji wao Yanga ambao waliweka kambi mkoani Morogoro wanatarajiwa kuwasili leo tayari kwa mchezo huo wa kukamilisha ratiba kwa upande wao.

USM Alger inasaka tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo na itafanikiwa kama itaibuka na ushindi au hata ikipata sare.

Wakati Yanga na USM Alger zikichuana kwenye uwanja wa Taifa, Gor Mahia na Rayon Sports zitakuwa zikichuana kwenye mchezo mwingine huko Kenya.

Gor Mahia ndio inaongoza msimamo wa kundi D ikiwa na alama nane sawa na USMA lakini Gor imefunga mabao mengi zaidi.

Rayon Sports iko nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu, inayo nafasi finyu ya kutinga robo fainali kama itashinda michezo yote miwili iliyobaki.

Yanga yenye alama moja haina nafasi ya kutinga robo fainali lakini itautumia mchezo huo kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara inayoanza wiki ijayo.

Pia mchezo huo utatumika kumuaga mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' ambapo wanachama na mashabiki wa Yanga mkoa wa Dar es salaam watapata nafasi ya kumuaga mkongwe huyo aliyetundika daruga na kukabidhiwa majukumu ya Umeneja wa Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’