kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omari Kaaya amesema wameanza mchakato wa uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Kaaya amesema hivi karibuni Yanga inatarajia kuitisha uchaguzi kujaza nafasi zilizowazi baada ya viongozi kujiuzulu.
Baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga, nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti zote ziko wazi.
Yanga pia inahitaji kujaza nafasi zilizoachwa na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji na Mashindano ambao nao walijiuzulu.
Hivi karibuni Shirikisho la soka nchini (TFF) liliviagiza vilabu vya Yanga na Simba kuhakikisha vimefanya uchaguzi katika muda wa siku 75.

ADVERTISE HERE