Uongozi wa klabu ya Yanga umewahimiza wanachama na mashabiki wa timu hiyo waendelee kuichangia timu yao.
Zoezi la uchangishaji lilianza siku nane zilizopita ambapo katika muda huo jumla ya Tsh 3,073, 263 zimechangishwa.
Mwamko wa uchangiaji unaonekana kuwa mdogo hivyo kuna umuhimu kwa WanaYanga kuhamasishana ili kuongeza kasi ya uchangiaji wa timu.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya amesema wataendelea kupokea michango ya WanaYanga bila ya kujali kiasi kinachopatikana.
Amesema pesa inayopatina itasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zinazoikabili timu.

ADVERTISE HERE