Katika kuhakikisha Yanga inakuwa na ukuta imara, Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania bara, Mwinyi Zahera amembadilishia majukumu beki Abadallah Shaibu 'Ninja'.
Katika mchezo wa jana dhidi ya Mawenzi Market, Shaibu aliyerithishwa jezi namba 23 na Nadir Haroub 'Cannavaro', alicheza namba sita akishirikiana na viungo Papi Tshishimbi na Feisal Salum 'Fei Toto'.
Hata hivyo Shaibu alicheza kwa kipindi kimoja tu na nafasi yake kuchukuliwa na Raphael Daudi baada ya kuumia kwenye kipindi cha pili.
Zahera amevutiwa na uwezo wa Shaibu katika ukabaji na kwa kumtumia mbele ya walinzi wa mwisho ataongeza ugumu kwa safu ya ulinzi ya Yanga kupitika kirahisi
Lakini pia uwepo wake utawapunguzia majukumu ya ukabaji Tshishimbi na Fei Toto ambao watabaki na majukumu zaidi ya kuchezesha timu.

ADVERTISE HERE