Wosia wa Nadir kwa wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Aug 2018
Wosia wa Nadir kwa wachezaji Yanga
Jana mkongwe Nadir Haroub aliagwa rasmi na Yanga baada ya kufikia tamati ya utumishi wake wa miaka 12 katika klabu hiyo.

Tukio hilo la aina yake lilifanywa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Ni katika uwanja huo Nadir alicheza mchezo wake wa kwanza alipojiunga na Yanga mwaka 2006.

Cannavaro amedumu Yanga kwa miaka 12. Hakika sio jambo rahisi na ni wachezaji wachache sana duniani wanaofanikiwa kuweka rekodi kama hiyo.

Cannavaro ametaja sababu kuu zilizomfanya adumu Yanga kwa muda mrefu kuwa ni uvumilivu na nidhamu.

"Kuwa na nidhamu na uvumilivu ndio siri ya mafanikio yangu," amesema Cannavaro.

"Nilimheshimu kila mmoja bila ya kujali umri, kipato au umaarufu. Niliwaheshimu walimu na nilifuata maelekezo waliyonipa"

"Nikiwa hapa kwa nyakati tofauti nilipitia changamoto nyingi za aiana tofauti, lakini nilivumilia"

"Lakini pia nilishirikiana na wachezaji wenzangu na sikusita kusikiliza maoni na ushauri wao," alisema Cannavaro

Uongozi wa Yanga ulimteua Nadir kuwa Meneja wa klabu hiyo huku aliyekuwa Meneja wa muda mrefu Hafidh Saleh kukabidhiwa majukumu mapya ya Uratibu.

Nadir amefichua siri kwamba ni wachezaji wa Yanga ndio waliopendekeza apewe majukumu hayo ya Umeneja.

Hili linadhihirisha kwamba Nadir ambaye alikuwa nahodha wa Yanga kwa miaka mitano, alifanya mambo mema yaliyowashawishi wenzake kutaka aendelee kubaki kwenye ngazi ya uongozi baada ya kustaafu.

Nadir sasa atakuwa daraja kati ya wachezaji na uongozi wa Yanga. Anazifahamu changamoto zao kwa kuwa yeye ameziishi kwa muda mrefu.

Lakini pia uzoefu wake utawasaidia baadhi yao wenye ndoto za kufanikiwa kama yeye.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’