Baadae leo kikosi cha Yanga kinashuka kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kuumana na Mawenzi Market katika mchezo maalum wa kumuaga mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' aliyestaafu.
Hii ni siku ya kipekee kwa WanaYanga kumuenzi Nadir, nahodha aliyeitumikia Yanga kwa muda mrefu zaidi.
Nadir amekuwa kwenye kikosi cha Yanga kwa zaidi ya miaka 12, akifanikiwa kushinda jumla ya mataji 16.
Ndiye mchezaji aliyeshinda mataji mengi zaidi katika historia ya Yanga akifuatiwa na Kitwana Manara 'Computer' na Abeid Mziba.
WanaYanga tunapaswa kuipa heshima ya kipekee siku ya leo kwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Jamhuri huku tukivalia T-Shirt rasmi zilizoandaliwa kwa ajili ya tukio hilo.
T-Shirt zinauzwa nje ya uwanja wa Jamhuri pia zinapatikana madukani.

ADVERTISE HERE