Zahera awafungia kazi Buswita, Ajib

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Aug 2018
Zahera awafungia kazi Buswita, Ajib
Hakuna asiyeujua uwezo wa viungo washambuliaji wa Yanga Pius Buswita na Ibrahim Ajib waliotua msimu uliopita wakitoka vilabu vya Mbao FC na Simba.

Ukizungumzia wachezaji wenye vipaji kwenye kikosi cha Yanga huwezi kukwepa kutaja majina ya viungo hao.

Kuhakikisha wanainufaisha Yanga msimu ujao, Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania Bara, Mwinyi Zahera amepania kuwaimarisha zaidi.

Zahera amekuwa akimpa mazoezi maalum Buswita kuhakikisha anaendana na mfumo wake.

Tangu kuwasili kwa Zahera, Buswita amekuwa akitumika kama kiungo zaidi tofauti na wakati wa Lwandamina ambapo alikuwa akitumika kama mshambuliaji msaidizi au winga.



Ajib alichelewa kujiunga na kambi ya Yanga mkoani Morogoro kutokana na matatizo ya kifamilia, hata hivyo baada ya kutua tu amekumbana na program maalum ya mazoezi ya peke yake.

Msimu uliopita Ajib aliifungia Yanga mabao sita kwenye duru ya kwanza hata hivyo alipoteza makali yake na kufunga bao moja pekee kwenye duru ya pili.

Majeraha pamoja na matatizo ya kifamilia ya mara kwa mara, zinatajwa kuwa sababu zilizopelekea kiwango cha Ajib kuporomoka mwishoni mwa msimu uliopita.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’