Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ana shauku kubwa ya kuiona timu yake ikicheza michezo zaidi ya kirafiki kabla ya kuivaa USM Alger Jumapili ya August 19, 2018.
Jana Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzanite Academy na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 lakini Zahera amesema haitoshi anataka mechi ngumu zaidi.
Yanga huenda ikacheza na Lipuli FC keshokutwa Jumamosi kabla ya mchezo wa kumuaga Cannavaro utakaopigwa Jumapili kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Baada ya mazoezi mfululizo ya wiki nzima, kikosi cha Yanga kinaonekana kuimarika.

ADVERTISE HERE