Klabu ya Simba leo ilifanya tamasha lake la kila mwaka linalofahamika kama Simba Day uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika kuhitimisha Tamasha hilo, Simba ilicheza na Asante Kotoko kutoka Ghana na kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Lakini mapema kabla ya mchezo huo, kwenye moja ya matukio, mkongwe Sunday Manara 'computer' alidhihirisha kuwa yeye ni Yanga Damu pale alipomkatalia katakata mwanawe Haji Manara kumvalisha jezi ya Simba.
Kwa wale wasiofahamu, Sunday Manara ndiye baba mzazi wa Haji Manara Afisa wa Habari wa Simba.
Haji alimtambulisha uwanjani mzazi wake huyo ambaye aliitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa miaka ya sabini sambamba na mkongwe Abdallah Kibadeni wa Simba.
Lengo la utambulisho huo lilikuwa kudumisha uhusiano mwema baina ya Yanga na Simba lakini pia kuweka msisitizo kuwa vilabu hivi si mahasimu bali ni watani wa jadi.
Lakini baadae Haji akajaribu kugeuza tukio hilo pale alipotaka amvalishe Baba yake jezi ya Simba huku akidai 'anamsilimisha'
Mzee Manara alikataa katakata huku akiigusa jezi yake ya Yanga aliyoivaa kuonyesha kuwa yeye ni Yanga Damu.

ADVERTISE HERE