Mapema leo kikosi cha Yanga kinachojifua mkoani Morogoro kilicheza mchezo wa kirafiki ambao ulikuwa sehemu ya mazoezi dhidi ya Academy ya michezo ya Tanzania na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1.
Heritier Makambo, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Emanuel Martin na Pius Buswita walipachika mabao hayo ya Yanga.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mchezo huo ulikuwa sehemu ya mazoezi ya kikosi chake na angependa kucheza mchezo mwingine wa kirafiki na timu ngumu zaidi kabla ya kuikabili USM Alger, August 19.
Jumapili, August 12 Yanga itacheza na Mawenzi Market katika mchezo wa kumuaga mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' alistaafu na sasa akiwa Meneja wa Yanga.

ADVERTISE HERE