Yanga imepania kuwanyamazisha 'wanaochonga sana'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Aug 2018
Yanga imepania kuwanyamazisha 'wanaochonga sana'
Licha ya kelele nyingi za kuibeza Yanga huko mtaani kutoka kwa wapinzani wao, kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara kinaendelea kujifua mkoani Morogoro.

Yanga tayari imetimiza wiki moja tangu itue mkoani humo kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara ikitarajiwa kuanzia ugenini kwa kucheza na Mtibwa Sugar, August 23 uwanja wa Jamhuri.

Pia Yanga itakuwa na kibarua cha kukamilisha ratiba ya michezo miwili ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger (August 19) na Rayon Sports (August 28).

Kwa maana kwamba Yanga itacheza na USM Alger kwenye uwanja wa Taifa kisha kurudi mkoani Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar siku tatu baadae.

Kocha aridhishwa na maandalizi

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema baada ya kukinoa kikosi chake kwa wiki moja, amevutiwa na mwitikio wa wachezaji kwa mazoezi anayowapa.

Zahera amesema ana uhakika kikosi chake kitakuwa imara zaidi ligi itakapoanza.

Ikumbukwe kabla ya kuivaa Gor Mahia, Yanga ilifanya maandalizi ya 'kimagumashi' huku ikiwa na wachezaji pungufu kufuatia wengine kugoma wakishinikiza wapewe mikataba.

Baadhi ya wachezaji walicheza michezo hiyo bila ya kuwa na mikataba.

Lakini sasa Zahera amesema wachezaji wote mawazo yao yako kwenye kucheza soka na ndio maana timu imeimarika kwa haraka.

Wachezaji wamepania kuwanyamazisha wakosoaji

Ari ya wachezaji wa Yanga iko juu sana wakati huu wakiwa na shauku ya kusahihisha matokeo mabaya mfululizo waliyopata.

Wachezaji wanayasikia hayo yanayosemwa mtaani na wamepania kuyajibu yote dimbani ligi itakapoanza.

Kwa kiasi kikubwa benchi la ufundi na viongozi wa Yanga wamefanikiwa kurejesha utulivu kwa wachezaji hivyo kuwafanya wafikirie zaidi kuipigania Yanga.

Yapania kutumia ipasavyo mapumziko ya kutoshiriki michuano ya CAF

Kwa zaidi ya misimu mitano mfululizo Yanga imekuwa ikikabiliwa na ratiba ngumu kutokana na ushiriki wake katika michuano ya ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho.

Wakati mwingine timu inapokosa nafasi ya kushiriki michuano hiyo, inapata muda wa kujipanga na inaweza kufanya vizuri zaidi katika ligi ya ndani.

Yanga ikishakamilisha mchezo dhidi ya Rayon August 23, itakuwa na ratiba ya michezo ya ligi pekee kabla ya kuanza kwa kombe la FA.

Na hili ndilo linalowafanya wachezaji waandamizi wa Yanga kuamini wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu ujao kama watajipanga vizuri.

Katika moja ya mahojiano yake, nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul alisema wanajiona wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya kurejesha ubingwa Jangwani na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya CAF mwakani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’