Mchezo wa Kagera vs Yanga waahirishwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Aug 2018
Mchezo wa Kagera vs Yanga waahirishwa
Mchezo wa raundi ya pili wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Kagera Sugar dhidi ya Yanga uliokuwa upigwe August 25 umeahirisha kutokana na Yanga kukabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports August 28, 2018.

Yanga itaanzia mkoani Morogoro August 23 kwa kucheza na Mtibwa Sugar kisha kusafiri nchini Rwanda kumenyana na Rayon.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura amesema mchezo huo wa raundi wa pili utapigwa mwezi Novemba 2018.

Kumekuwa na malalamiko kwa ratiba hiyo kuwa imetoa upendeleo kwa Simba ambayo itaanzia nyumbani kwa kucheza michezo minne mfululizo huku timu nyingine ikiwemo Yanga zikipangiwa michezo mitatu mfululizo ugenini.

Msingi wa malalamiko hayo pia unabebwa na utaratibu mpya wa mapato msimu huu ambapo timu mwenyeji itachukua mapato yote.

Ratiba hiyo itaziumiza zile timu zilizopangiwa kucheza michezo mingi mfululizo mwanzoni kwani zitalazimika kusaka fedha za kuwezesha kusafirisha timu pamoja na mahitaji mengine.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’