Katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga Charles Mkwasa yuko nchini India akiendelea na matibabu ya maradhi yanayomsumbua.
Mkwasa aliondoka nchini kwenda India mapema wiki iliyopita baada ya kubainika kuwa na matatizo ya moyo.
Mkwasa alijiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Yanga baada ya kukumbwa na maradhi hayo yaliyoathiri mfumo wake wa upumuaji.
Kiongozi huyo ambaye pia amewahi kuitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa akiwa mchezaji mwishoni mwa miaka ya 70 na mwanzoni mwa miaka ya 80, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Tunamtakia kila la kheri katika matibabu yake ili aweze kurudi salama kuendelea na majukumu mengine ya ujenzi wa Taifa.

ADVERTISE HERE