Ngassa anasema Yanga itatisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
5 Aug 2018
Ngassa anasema Yanga itatisha
Winga wa Yanga, Mrisho Ngassa ameupongeza uongozi wake kwa kufanya usajili wa maana, huku akiwatuliza mashabiki wa klabu hjiyo kuwa pamoja na ukata unaowakabili timu hiyo bado itafanya maajabu katika Ligi Kuu Bara 2018-2019.

Ngassa ambaye yuko kambini mkoani Morogoro na kikosi hicho, amesema alikuwa akifanya mazoezi na wachezaji wachache, lakini tangu aingie kambini amegundua Yanga ina kikosi kizuri kitakacholeta ushindani kwa wapinzani wao.

“Kumekuwa na maneno mengi, eti Yanga haiwezi kufanya vizuri kwa usajili wa kawaida iliyofanya, wacha waendelee kujidanganya ila tupo vizuri na mashabiki wasubiri waone mambo wasitishwe na majina ya timu nyingine,” alisema Ngassa.

Ngassa aliyeichezea Yanga kwa mafanikio kabla ya kutimka mwaka 2015 kwenda Afrika Kusini, alisema timu yao imetawala chipukizi wengi wenye uchu wa mafanikio, hivyo anaamini wakishirikiana na wazoefu wataifanya timu iwe tishio.

Aliongeza mpira unachezwa hadharani sio wa kujificha, hivyo hawezi kutumia maneno sana kufikisha ujumbe kwa mashabiki kubwa aliwaomba waachane na matokeo mabaya ya timu yao katika mashindano ya kimataifa huku akiwataka kuwaombea waweze kuwa fiti zaidi kuelekea msimu mpya.

“Mashindano ya kimataifa kwa sasa ni ukamilikaji wa ratiba kwa upande wa timu yangu kwani hata wakishinda michezo yote iliyosalia haifiki popote. wanatakiwa kusahau matokeo ya nyuma tuangalie tunajipangaje kwa msimu mpya,” alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →