Huyo Makambo amepania kweli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Aug 2018
Huyo Makambo amepania kweli
Mshambuliaji mpya wa Yanga Heritier Makambo amesema atahakikisha anafunga mabao mengi ili kuiwezesha Yanga kufanya vizuri msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom.

Makambo ambaye yuko kwenye kikosi cha Yanga kilichoweka kambi mkoani Morogoro kikijifua katika uwanja wa SUA amesema kucheza Yanga ni kutimiza ndoto aliyokuwa nayo kwa muda mrefu.

Makambo amesema ameifahamu Yanga muda mrefu, ndio timu kubwa kutoka Tanzania aliyokuwa akiifahamu wakati akiwa kwao DR Congo.

Mshambuliaji huyo aliyetua Yanga kutoka FC Lupopo amekuwa akionyesha mambo makubwa kwenye mazoezi na kuwapa matumaini mashabiki wanaofurika kushuhudia mazoezi mkoani Morogoro.

Ili kuhakikisha anaanza kuitumikia Yanga mapema, viongozi wa Yanga wanahaha kupata uhamisho wake wa Kimataifa (ITC) kutoka DR Congo

Makambo na mlinda lango Klaus Kindoki ndio wachezaji pekee wa kigeni ambao wamesajiliwa na Yanga msimu huu na bado ITC zao hazijafika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’