Zahera ataka aongezwe watatu wa kigeni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Aug 2018
Zahera ataka aongezwe watatu wa kigeni
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewataka mabosi wa mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania Bara kuhakikisha wanasajili wachezaji watatu kabla dirisha la usajili wa wachezaji wa kigeni halijafungwa.

Dirisha la usajili wa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 06, hivyo Yanga inayo nafasi ya kuimarisha zaidi kikosi chake.

Zahera ambaye yuko mkoani Morogoro akiendelea na kambi, amesema kuna ulazima wa Yanga kusajili walinzi wawili, mmoja wa kati na mwingine upande wa kulia.

Lakini pia Mcongo huyo mwenye uraia wa Ufaransa ametaka kuongezwa mshambuliaji mwingine.

"Nimeambiwa bado kuna muda kidogo wa kusajili wachezaji wa kigeni sasa ukiangalia kikosi chetu tunahitaji straika mwingine bora kama Makambo," Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti

"Hilo nimewakabidhi viongozi pia kama watapata beki wa kati mmoja mwenye ubora kama Kelvin (Yondani) basi tutakuwa tumeboresha nafasi hiyo, nataka mtu wa kushindana na Kelvin (Yondani) pia unajua Kessy hatakuwepo ni vyema tukapata beki wa kulia atakayeshindana na Juma (Abdul).

"Ili uwe na timu nzuri inayoshindana ni vyema kila nafasi ukawa na watu wawili au zaidi ili ushindani uwepo ukiacha mtu mmoja ni rahisi mchezaji kubweteka na kuiangusha timu."

Baada ya kuvunja mkataba wa Youthe Rostand, Yanga imebaki na wachezaji watano wa kigeni ambao ni Klaus Kindoki, Thabani Kamusoko, Papi Tshishimbi, Amissi Tambwe na Heritier Makambo.

Inaweza kusajili hadi wachezaji watano wa kigeni ili kukamilisha ukomo wa wachezaji 10 walioruhusiwa na TFF.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’