Kikosi cha Yanga kiliondoka mapema leo kuelekea mkoani Morogoro kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya ligi pamoja na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika amesema timu imewasili salama mkoani humo na kesho itaanza rasmi mazoezi kulingana na program za kocha Mwinyi Zahera.
Msafara wa Yanga uliongozwa na Meneja Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Ikiwa mkoani Morogoro Yanga itacheza michezo kadhaa ya kirafiki huku August 12 ikitarajiwa kucheza mchezo maalum wa kumshukuru na kumuaga Nadir aliyestaafu na sasa kukabidhiwa majukumu ya Umeneja wa timu.
Yanga itacheza na USM Alger August 19 kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kurudi mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar August 23 ukiwa mchezo wa kwanza wa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom.

ADVERTISE HERE