Kama ulikuwa unadhani matokeo yasiyoridhisha iliyopata Yanga katika mashindano ya kimataifa yataendelea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, umekosea.
Mashabiki wa Yanga hawakielewi kikosi chao na wamekata tamaa baada ya kupata matokeo yasiyokuwa na tija katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga ina pointi moja katika kundi lake baada ya kucharazwa mabao 4-0 na USM Algier ya Algeria, ilitoka suluhu na Rayon Sports (Rwanda), ilinyukwa 4-0 na Gor Mahia (Kenya) katika mchezo wa awali kabla ya kulala 3-2 ziliporudiana.
Timu hiyo inayonolewa na kocha raia wa DRC Mwinyi Zahera, imebakiza mechi mbili dhidi ya USM Algier kabla ya kuivaa Rayon Sports.
Matokeo hayo yamewakatisha tamaa mashabiki wa klabu hiyo ambao wameingiwa hofu kama timu hiyo itacheza kwa kiwango bora mechi za Ligi Kuu msimu ujao.
Pamoja na hofu hiyo, Zahera amewataka mashabiki kujiandaa kucheka kwa kuwa ana mkakati imara wa kuipa mafanikio Yanga.
Zahera alisema ana uhakika kabla ya Ligi Kuu kuanza Agosti 22, Yanga itakuwa imerejesha makali yake kwa kuwa wachezaji watakuwa kwenye ubora wao.
“Ligi Kuu ikianza hatutakuwa katika ubora huu tutakuwa na timu tofauti, tutakuwa na timu yenye sura nzuri kwa ushindani, kuna wachezaji tumewasajili wataleta kitu tofauti kabisa,”alisema Zahera.
Kocha huyo alisema anaamini Yanga ina wachezaji hodari watakaoivusha katika Ligi Kuu licha ya kutopewa nafasi ya kufanya vyema.
Alitaja mkakati wake katika maandalizi ya ligi kuwa ni kuingia kambini mapema ili kujenga timu imara yenye ushindani.
Akizungumzia mechi mbili za kimataifa zilizobaki dhidi ya USM Algier na Rayon Sports, kocha huyo alidai Yanga haiwezi kufanya maajabu kwa kuwa tayari timu hiyo imepoteza nafasi ya kufuzu robo fainali.
“Angalia nahitaji kitu fulani kutoka kwa Ngasa, lakini hatuwezi kumtumia kama ilivyokuwa kwa Jafari, Banka, Makambo, Kindoki na Feisal hawa ni wachezaji wenye ubora mkubwa ambao wangetuongezea nguvu ya ushindani,” alisema Zahera.
Alisema akiangalia kisaikolojia wachezaji wake hawako sawa na kwamba hilo linatakiwa kufanyiwa kazi na uongozi wa klabu yao kabla ya kuanza kwa maandalizi ya mwanzo wa msimu.
Tangu kuondoka kocha George Lwandamina Yanga imecheza mechi 13, imeshinda dhidi ya Mbao, ilitoka sare mara nne na imepoteza mechi nane.
Zahera anatarajiwa kukaa kwenye benchi kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kimataifa dhidi ya USM Alger Agosti 19.
Alisema Yanga imefanya usajili mzuri, lakini baadhi ya wachezaji wake hawako kwenye kiwango kizuri na wengine hawezi kuwatumia kwa kuwa hawapo katika usajili wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Yanga imewasajili winga mkongwe Mrisho Ngassa, washambuliaji Heritier Makambo na kipa Klaus Kindoki (DR Congo), viungo Mohammed Issa ‘Banka’ (Mtibwa), Feisal Salum (JKU Zanzibar), Jafary Mohammed (Majimaji) na Deus Kaseke (Singida United).
Kwa nyakati tofauti wachezaji wa Yanga waliwatoa hofu mashabiki wao wakisisitiza kuwa Yanga itakavyoanza msimu mpya itakuwa tofauti na vile inavyodhaniwa.
Kipa wa Yanga, Beno Kakolanya alisema, Yanga ina kikosi imara ambacho kina uwezo wa kucheza kwa kiwango bora msimu ujao.
“Watu wasichukulie Yanga kawaida kutokana na matokeo ya kimataifa tuliyopata, kwenye ligi, Yanga itakuwa ya tofauti na inavyodhaniwa, acha benchi la ufundi lifanye kazi yake,” alisema Kakolanya.
Beki Andrew Vincent ‘Dante’ alisema walifanya makosa kwenye mashindano ya kimataifa, lakini hayatajirudia kwenye Ligi Kuu.
“Kilichotokea ni makosa ya kimpira na mengine yalichangiwa na vitu vingi, kwa sasa timu imetulia tunajipanga kwa Ligi Kuu, upande wa pili wasifikirie kwamba matokeo ya mechi za kimataifa ndiyo yatageukia kwenye ligi,” alisema Dante.
Naye mshambuliaji mahiri wa timu hiyo Amissi Tambwe, alisisitiza kuwa nia yao ni kupigania ubingwa wa Ligi Kuu na siyo vinginevyo kwa sasa.
Alisema wanayanga watafurahia vitu watakavyovifanya kwa kuwa kila mchezaji ameumizwa na matokeo mabaya waliyoyapata kwenye Kombe la Shirikisho hivyo mkakati wao ni kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE