Dante anasema mbona 'beki mbili' anapiga 'fresh' tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
2 Aug 2018
Dante anasema mbona 'beki mbili' anapiga 'fresh' tu
Beki Andrew Vincent ‘Dante’ anayekipiga katika klabu ya Yanga, amewatuliza mashabiki wa timu yake kwamba ikitokea beki mwenzake Juma Abdul amepata tatizo katika msimu ujao anaweza kuziba pengo hilo bila wasiwasi.

Katika nafasi ambayo anacheza Juma Abdul (beki wa kulia) awali alikuwa anacheza na Hassan Kessy, lakini Kessy aliondoka kikosini hapo baada ya kushindwa kuafikiana katika suala zima la maslahi ya mkataba mpya hali iliyofanya kubaki Abdul pekee katika nafasi hiyo.

Dante ameuambia mtandao wa Mwanaspoti kwamba iwapo itatokea tatizo katika nafasi ya beki wa kulia basi anaweza kuziba pengo kwani nafasi hiyo alikuwa akiicheza mara kwa mara alipokuwa Mtibwa Sugar.

“Ninja anazidi kukomaa kadri siku zinavyosonga mbele na hilo ni jambo bora kwani itazidi kuongeza utulivu safu yetu ya ulinzi, ikitokea Juma kapata tatizo mimi nitacheza nafasi ile kwasababu nilipokuwa Mtibwa nilikuwa naicheza nafasi hiyo nakumbuka mechi dhidi ya Yanga, niliweza kupambana na Andrey Countinho vizuri kwahiyo wasiwe na wasiwasi,” alisema.

Akizungumzia kikosi chao katika msimu ujao, alisema watu wengi wamekuwa wakiwaangalia kwa uoga na kuona kama watakuwa wasindikizaji kitu ambacho ni tofauti.

“Unajua katika mashindano mengine kiukweli ile kwenda na kurudi nayo ilichangia kwasababu wachezaji tulikuwa hatupati kitu sawa," amesema.

"Naamini kabisa tukikaa kwa pamoja katika maandalizi ya Ligi Kuu basi tutaonyesha kitu cha tofauti, hilo hata katika mechi ya marudiano dhidi ya Gor Mahia limeonekana kwasababu maandalizi ya mechi ya kwanza na ya marudiano ni tofauti hata mchezo ulivyokuwa hapa nyumbani ulionekana,” alisema.

Yanga inaondoka leo kuelekea mkoani Morogoro kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi 22 Agosti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →