Michango ya mashabiki haitatosha kuiendesha Yanga, twendeni kwenye mabadiliko

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
1 Aug 2018
Michango ya mashabiki haitatosha kuiendesha Yanga, twendeni kwenye mabadiliko
Jana Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya alieleza kuwa timu hiyo inaandaa mpango wa kuwawezesha wadau, wanachama na mashabiki wake kuweza kuichangia fedha ili iweze kujiendesha.

Kaaya alisema wakati huu Yanga inapitia changamoto nyingi za kiuchumi ambazo zinahatarisha timu hiyo kushindwa kutekeleza baadhi ya mipango yake.

Sasa badala ya mashabiki kulalamika tu, wameombwa kuwajibika kwa kuchangia fedha za kuwezesha kukamilishwa kwa baadhi ya mipango.

Hata hivyo mpango huu sio wa kudumu na viongozi wa Yanga watafanya makosa makubwa kama wanafikiria timu itaweza kujiendesha kwa kutegemea michango ya mashabiki wake.

Hapo nyuma Yanga iliwahi kuendesha mchakato huo lakini ulikufa kimyakimya kwani mapato yaliyokuwa yakipatikana hayakutosheleza kumaliza changamoto zinazoikabili Yanga.

Yanga ni taasisi kubwa, litakuwa jambo la aibu kwa taasisi hii kuendeshwa kwa michango ya mashabiki wake pekee.

Viongozi wa Yanga ni vyema wakafikiria miradi mikubwa itakayokuwa na manufaa ya kudumu kwa klabu na sio miradi ya mda mfupi ambayo mwisho wake unaonekana hata kabla haijaanza.

Wengi wamesisitiza umuhimu wa kuharakisha mchakato wa mabadiliko. Hakuna muujiza ambao utaiondoa Yanga katika hali iliyonayo sasa kama viongozi waliopo hawako tayari kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Tangu mchakato huo ulipoanza mwaka jana, kama viongozi wangeweka msisitizo mchakato huo ungekuwa umekamilika na pengine wakati huu Yanga isingekuwa inapitisha bakuli kwa mashabiki wake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’