Klabu ya Simba jana imemtambulisha rasmi dimbani kiungo Haruna Niyonzima aliyepata mafanikio makubwa akiwa na Yanga kwa miaka sita.
Baada ya tafrija yao kumalizika jana, Niyonzima alizungumza na waandishi wa habari ambapo mbali na mambo mengine alitoa shukrani za pekee kwa klabu ya Yanga.
Niyonzima amekiri kwake yeye hakuna timu kama Yanga.
Amesema Yanga ni timu pekee aliyokaa kwa muda mrefu kuliko timu nyingine yoyote duniani na ameishuku Yanga kwa ushirikiano aliopatiwa kwa kipindi chote alichokuwa nasi.
Soka ni burudani na wala sio uadui hivyo nasi tunamtakia kila la kheri huo alikokwenda, lakini tunampa pole kwani itabidi azoee na kusahau kuhusu kutwaa ubingwa!
Ubingwa pekee wa Simba ni kupitia matamasha kama lile walilofanya jana Nane Nane Day!
Yanga itazidi kusonga mbele na kuendeleza desturi yake ya kutwaa mataji kila mwaka.
Wale wanaodhani Niyonzima ameacha pengo Yanga wasubiri msimu mpya wa ligi utakapoanza.

ADVERTISE HERE