Mashabiki, Wanachama Yanga watakiwa kuichangia timu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jul 2018
Mashabiki, Wanachama Yanga watakiwa kuichangia timu
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya amesema wako mbioni kukamilisha mchakato wa kuandaa namba maalum zitakazowawezesha wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuweza kuichangia timu yao.

Kaaya amesema mpango huo utawawezesha WanaYanga wote kuweza kuwajibika kuisaidia timu badala ya kuishia kulalamika tu.

"Ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazotukabili inatufaa kuwa kitu kimoja. Inatubidi tupate michango ya wadau wote wa Yanga bila ya kujali ni mwanachama, shabiki au mdau wa michezo," Kaaya ameiambia Azam TV.

"Yanga ni timu yetu sote, inapofanya vibaya tunaumia sote. Tusiishie kulaumu tu wakati hatutekelezi wajibu wetu ipasavyo."

"Tutatangaza namba ambazo tutazitumia kwa ajili ya kupata michango ya kila Mwana Yanga popote alipo"

"Tulikuwa na utaratibu huo zamani lakini haukuenda kama ulivyotarajiwa. Lakini wakati huu ni muafaka zaidi kwa kuwa tunahitaji msaada kutoka kwa Wana Yanga."

Kaaya amesema Yanga inahitaji michango ya wadau wake ili iweze kukamilisha michakato mbalimbali ikiwemo kuweka kambi nzuri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi Kuu na michezo iliyobaki ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’