Yanga iko imara, muhimu maandalizi tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jul 2018
Yanga iko imara, muhimu maandalizi tu
Wapo waliokata tamaa na Yanga kufuatia vipigo mfululizo kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Aidha pia wapo wenye mashaka na usajili wa wachezaji saba uliofanywa na timu hiyo kuwa huenda msimu ujao wa ligi hali itakuwa ngumu.

Lakini ukweli ni kwamba licha ya 'ukata' kuwa sababu kuu iliyopelekea 'ufinyu' wa usajili, Yanga bado ina kikosi imara na itafanya vizuri kwenye ligi msimu ujao.

Muhimu ni kwa viongozi wa mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara kuweka mkazo kwenye maandalizi ya kutosha.

Sasa zimesalia wiki tatu kabla ya ligi kuanza na ni vyema uongozi wa Yanga tayari umebainisha kuipeleka timu kambini mkoani Morogoro.

Licha ya Donald Ngoma na Obrey Chirwa kuondoka, Yanga imesajili mshambuliaji mmoja pekee, Heritier Makambo.

Lakini mshambuliaji Matheo Anthony ambaye ameimarisha kiwango chake ni kama amesahaulika.

Matheo atashirikiana kikamilifu na Makambo na mkongwe Amissi Tambwe kuibeba safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Yanga pia imeimarisha safu yake ya kiungo cha kati kwa kuwasajili Feisal Salum 'Fei Toto', Mohammed Issa 'Banka' na kiraka Jaffar Mohammed ambaye pia ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa pembeni.

Hawa wanaungana na Pius Buswita, Raphael Daudi na Thabani Kamusoko kuboresha zaidi safu ya kiungo.

Usajili wa Fei Toto na Banka ni wa maana sana kwani utaongeza ufundi na ubunifu katika uchezeshaji wa timu.

Baada ya msimu uliopita Kamusoko kupoteza makali yake kutokana na majeraha, Yanga ililazimika mara kwa mara kumtumia Tshishimbi kama kiungo mchezeshaji licha ya ukweli kwamba Mcongomani huyo alisajiliwa akiwa kiungo mkabaji.

Lakini sasa Yanga imefanya jambo la maana kumsajili Fei Toto kwani ni aina ya viungo wenye 'akili' na uwezo mkubwa wa kuchezesha timu.

Kwa waliofuatilia michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es salaam, waliona uwezo wa Fei Toto.

Hakuna shaka ujio wa kiungo huyo utamfanya kocha Mwinyi Zahera kumrejesha Tshishimbi kwenye namba yake ya kiungo mkabaji.

Katika namba hiyo pia atakuwa na chipukizi Maka Edward ambaye alionyesha ukomavu kwenye michezo ya mwishoni msimu uliopita.

Bila kumsahau Said Juma Makapu ambaye amekuwa akitumika kama kiungo au mlinzi wa kati kulingana na mahitaji.

Kwa ufupi ni kwamba msimu ujao Yanga haitakuwa na tatizo kwenye sehemu ya kiungo kwani ina idadi ya kutosha ya viungo.

Aidha ujio wa Deus Kaseke na Mrisho Ngassa utarejesha utamaduni wa Yanga wa kushambulia kupitia pembeni.

Hawa wataongeza changamoto kwa Yusufu Mhilu, Emanuel Martin, Ibrahim Ajib na Juma Mahadhi kuimarisha viwango vyao.

Mashaka makubwa yamekuwa kwenye safu ya ulinzi ambayo itawategemea zaidi Kelvin Yondani na Andrew Vicent Chikupe.

Lakini hata Abdallah Shaibu 'Ninja' ataweza kuwasaidia walinzi hao kadiri itakavyohitaji kwani ameendelea kuimarika kutokana na uozefu anaoupata kwenye michuano ya Kimataifa.

Mlinda lango Kalius Kindoki ni mgeni, bado hajafahamika makali yake.

Lakini kupona kwa Benno Kakolanya na uwepo wa Ramadhani Kabwili utatosha kurejesha imani ya mashabiki wa Yanga katika eneo la ulinzi wa lango bila kumtegemea Youthe Rostand.

Yanga pia imechukua hatua ya kubadili kocha wa makipa, Razak Siwa akitarajiwa kurithi mikoba ya Juma Pondamali
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’