Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika ametoa ufafanuzi wa sababu iliyopelekea kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kushindwa kukaa kwenye benchi licha ya kuelezwa kuwa kibali tayari kilikuwa kimepatikana.
Nyika amesema taratibu za uhamiaji ndizo zilizopelekea Zahera kukaa jukwaani kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Gor Mahia lakisi sasa kibali cha kocha huyo kiko tayari.
Pia amesema mchakato wa ufuatiliaji wa kibali hicho ulicheleshwa kwa kiasi kikubwa na changamoto zilizoukumba uongozi wa Yanga siku za hivi karibuni.
Nyika amesema mchakato huo ulikwama baada ya kuugua na kisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa.
Kaimu Katibu Mkuu Omary Kaaya aliyeteuliwa hivi karibuni ndiye aliyefanikisha kupatikana kwa kibali cha Zahera.

ADVERTISE HERE