Yanga imeweka hadharani muundo wa jezi za nyumbani na ugenini zitakazotumika msimu ujao na mabingwa hao wa Kihistoria wa soka la Tanzania Bara.
Kulingana na taarifa iliyotolewa mapema jana, jezi hizo zitaanza kuuzwa mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya Yanga.

Pia uongozi wa Yanga umeahidi kuandaa utaratibu 'rafiki' utakaowezesha jezi hizo kupatikana kwa urahisi kila pembe ya Tanzania.
Wakati timu ikipita katika mazingira magumu kutokana na ukosefu wa fedha, kama uongozi utasimamia vyema mauzo ya jezi, mapato yatapatikana ya kutosha.
Kinachozikwamisha timu za Tanzania, Yanga ikiwa mojawapo, ni kutokuwa na mifumo mizuri ya usimamizi wa bishara hiyo hivyo kuwapa mwanya 'wajanja' kuteka mchakato na kujinufaisha wao badala ya klabu.

ADVERTISE HERE