Hili la wachezaji kuchukuliwa kabla ya mechi jana limekaaje?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
30 Jul 2018
Hili la wachezaji kuchukuliwa kabla ya mechi jana limekaaje?
Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Mzambia Noel Mwandila jana alilalamikia kitendo cha Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuwaondoa wachezaji sita wa Yanga kambini juzi mchana na kuwarudisha usiku wa manane.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana baada ya mcheezo dhidi ya Gor Mahia uliomalizika kwa Yanga kufungwa mabao 3-2, Mwandila aliwataja wachezaji hao kuwa ni kipa Ramadhani Kabwili, beki Gardiel Michael na viungo Raphael Daudi, Ibrahim Ajib na Deus Kaseke.

Mwandila alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TFF, Aaron Nyanda aliondoka na wachezaji hao juzi saa 8:00 hoteli ya Zimbo, iliyopo makutano ya mitaa ya Ndovu na Nyamwezi na kuwarudisha saa 8:00 usiku wa kuamkia jana.

Pamoja na kumkatalia kwa sababu timu ilikuwa ina mechi jana, lakini Mwandila amesema Nyanda alisistiza kuwachukua kwa sababu walikuwa wanatakiwa kwenda kupiga picha maalum za wadhamini wa timu ya taifa, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

Lakini Mwandila amesema wachezaji hao walirudi baada ya saa 8:00 usiku tena baada ya Mratibu wa Yanga SC, Hafidh Saleh kumpigia simu Nyanda kulalamikia kuchelewa kwa wachezaji hao.

“Kulikuwa kuna haraka gani ya kuwachukua wachezaji hao jana, kwa nini wasingesubiri tumalize mechi. Lakini mbona wachezaji wengine wote wa timu ya taifa hawakuchukuliwa kutoka Azam, Simba wapo Uturuki na timu za mikoani. Kwa nini ilikuwa Yanga tu,”alihoji Mwandila.

Mzambia huyo alisema mambo ya aina hiyo huwezi kustaajabu soka ya Tanzania iko chini, kwa sababu badala ya viongozi wa TFF kuzisaidia klabu zifanye vizuri kwenye mashindano zinashiriki kuzididimiza.

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →