Katika ligi za huko nje tumeshuhudia timu zikiwaaga wachezaji wao waandamizi kwa heshima wakati mwingine wakiandaa michezo maalumu kwa ajili yao.
Uongozi wa Yanga jana ulitangaza kuwa Nadir Haroub 'Cannavaro', nahodha na mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu zaidi, atakuwa Meneja mpya wa kikosi hicho.
Nadir amehitimisha miaka 12 ya maisha yake akiwa mchezaji wa Yanga. Aliingia Yanga akiwa bado kijana wa miaka 24 na sasa amestaafu akiwa na miaka 36.
Wadau wanadhani kwa heshima aliyoipa Yanga, Nadir hatakuwa amefanyiwa uungwana kama hataandaliwa jambo kubwa litakalobaki katika kumbukumbu ya maisha yake na klabu ya Yanga pia.
Kwa soka la Tanzania si rahisi kwa mchezaji kudumu kwenye klabu moja kwa miaka 12. Ni yeye aliyefanya hivyo akivunja rekodi ya Fred Mbuna aliyedumu Yanga kwa miaka 11.

ADVERTISE HERE