Yanga imeiva - Lwandamina

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
9 Aug 2017
Yanga imeiva - Lwandamina
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amejiridhisha kuwa mazoezi ya kujenga miili aliyokipa kikosi chake kwa takribani wiki tatu yamekuwa na faida.

Yanga ilianza na mazoezi ya Gym kwa wiki mbili na kisha kwenda kuweka kambi ya siku 10 mkoani Morogoro.

Yanga inaendelea kujifua jijini Dar es salaam uwanja wa Polisi, Kurasini.

Katika mazoezi ya sasa muda mwingi kikosi cha Yanga kinatumia kucheza mpira ambapo kocha Lwandamina pamoja na msaidizi wake Shedrack Nsajigwa wamekuwa wakitoa maelekezo ya kiufundi.

"Yale mazoezi ya Gym yalikuwa maalumu kuwaweka vijana tayari kwa msimu mpya," amesema Lwandamina.

"Mara nyingi yanafanywa mwanzoni mwa msimu ili kuwaongezea wachezaji ari, nguvu na kuwaepusha na majeraha ya kizembe."

"Vijana wanaonekana kuwa tayari na hivi sasa tunawaweka sawa kuendana na mifumo ya uchezaji tunayotaka. Baadhi ya wachezaji ni wapya, hatukuwa nao msimu uliopita, tunahitaji kuwaunganisha na wenzao."

Yanga imeongeza wachezaji wapya nane ambao ni Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, Pius Buswita, Raphael Daudi, Abdallah Shaibu, Gadiel Michael, Ibrahim Ajib na Papi Kabamba.

Aidha Yusuph Mhilu, Said Mussa na Maka Edward wao wamepandishwa kutoka kikosi cha pili cha Yanga (Yanga B).
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’