Mawindo ya Gor Mahia yanaendelea Kurasini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jul 2018
Mawindo ya Gor Mahia yanaendelea Kurasini
Yanga imeendelea kujifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga imeongezewa nguvu baada ya CAF kuthibitisha usajili wa mshambuliaji Matheo Antony na kiungo Deus Kaseke.

Wawili hao wanaweza kucheza dhidi ya Gor Mahia Jumapili.

Pia kurejea kwa beki Kelvin Yondani kutaimarisha safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara.

Bado hatma ya beki Hassani Kessy haijafahamika, huku kukiibuka taarifa kuwa huenda Kessy akatimkia nchini DRC.

Ingawa Yanga haijawa na maandalizi ya kutosha kutokana na migogoro ya hapa na pale, mchezo dhidi ya Gor Mahia utatoa hatma yake kwenye michuano hiyo.

Kama Yanga itashinda, itaweka hai matumaini ya kutinga robo fainali. Lakini kama itatoka sare au hata kufungwa basi itasubiri kukamilisha ratiba kwa michezo miwili itakayokuwa imebaki.

USM Alger inaongoza kundi D ikiwa imejikusanyia alama saba, inafuatiwa na Gor Mahia yenye alama tano.

Rayon Sports iko nafasi ya tatu ikiwa na alama mbili wakati Yanga iko nafasi ya nne ikiwa na alama moja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’