Kaaya aahidi kurejesha utulivu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
25 Jul 2018
Kaaya aahidi kurejesha utulivu Yanga
Kaimu Katibu Mkuu mpya wa Yanga, Omari Kaaya ametangaza kufanya maajabu ndani ya saa 48 zijazo kwa kuirejesha klabu hiyo katika hali ya utulivu.

Kauli ya Kaaya imekuja kutokana na Yanga kulazimika kufanya usajili wa wachezaji wake ndani saa 24 kabla ya kufungwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kaaya alitangazwa jana kujaza nafasi ya Charles Mkwasa, aliyetangaza kujiuzulu wadhifa wake kwa sababu za afya. Mbali na Mkwasa, Yanga pia ilimpoteza Makamu Mwenyekiti wake Clement Sanga, aliyejiuzulu kwa madai ya kutishiwa kuuawa.

Sanga anaungana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga kujiuzulu akitanguliwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Ayoub Nyenzi, Hashimu Abdallah, Salum Mkemi na Omari Saidi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, alimtangaza Kaaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu baada ya kudumu katika wadhifa wa ofisa masoko ndani ya klabu hiyo.

Ten alisema Wajumbe wa Baraza la Wadhamini walipitisha jina la Kaaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga.

Kaaya alisema jukumu lake la kwanza baada ya kupewa kazi hiyo ni kuhakikisha ndani ya saa 48 zijazo, wachezaji wote watakuwa wametia saini mikataba ya kuitumikia Yanga msimu ujao.

Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika ni Kelvin Yondani, Hassani Kessy, Juma Abdul, Benno Kakolanya na Geofrey Mwashiuya.

Pia alisema atahakikisha Yanga inacheza kwa kiwango bora mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Jumapili wiki hii.

Yanga inatakiwa kushinda mchezo huo ili kufufua matumaini ya kusonga mbele baada ya kulala mabao 4-0 ugenini kwenye Uwanja wa Kasarani, Kenya.

“Nimekubali kuvaa viatu vya Mkwasa (Charles), nina jukumu zito sana hasa hili la usajili, kuna baadhi ya wachezaji mikataba yao imemalizika na tunawahitaji watie saini tena.

“Wachezaji wengine wapya wanatakiwa kusajiliwa, ni kipindi kigumu lakini nitajitahidi kupitia kamati zilizopo na wadau wengine kukamilisha zoezi hili gumu,” alisema Kaaya.

Yanga imekumbwa na mtikisiko wa kiuchumi tangu alipojiweka kando Manji.

Klabu hiyo inapitia kipindi kigumu, baada ya kuyumba kiuchumi hatua iliyochangia kufanya usajili wa kusuasua licha ya kubakiwa na saa 48 kabla ya dirisha kufungwa kesho saa sita usiku.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →