Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia leo Julai 24,2018 ametoa ufafanuzi kuhusu kanuni ya kusajili wachezaji 10 wa kigeni.
Karia amesema baada ya mapendekezo ya klabu kuwasilishwa ilionekana ni kanuni itakayolinda wachezaji wazawa na kuwa na wachezaji bora wenye viwango.
Amesema kama kanuni hiyo itaonekana kuwa na athari TFF inatoa nafasi ya kukaa chini na klabu ili kuifanyia mabadiliko lakini kwa msimu huu wa 2018/2019 kanuni hiyo itabaki kama ilivyopitishwa.
Kumekuwa na mjadala miongoni mwa wadau wa soka nchini wengi wakionyesha hofu yao juu ya athari inayoweza kusababishwa na kanuni hiyo hasa kwa timu ya Taifa.
Juzi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe aliitaka TFF itoe ufafanuzi juu ya uamuzi wa ongezeko hilo la wachezaji wa kigeni

ADVERTISE HERE