TFF bado inamtambua Manji kama Mwenyekiti wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
24 Jul 2018
TFF bado inamtambua Manji kama Mwenyekiti wa Yanga
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameshangazwa na mwenendo wa viongozi wa Yanga kujiuzulu mfululizo, huku akisema anawakaribisha viongozi waliobaki ili kuweza kujadili.

Karia alisema, "Hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kutokea hali hii, iliwahi kutokea kwa Nchunga lakini awali tuliwahi kuwaita pamoja na Coastal Union lakini hawakuja ila Coastal walikuja na wamefanikiwa kufanya uchaguzi wao," alisema

Karia aliongeza kwamba mpaka hivi sasa wanatambua kwamba Mwenyekiti wa Yanga ni Yusuph Manji baada ya Klabu ya Yanga kupeleka barua katika shirikisho hilo.

Awali jana Jumatatu, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alitangaza kujiuzulu wadhifa wake, huku wadau wa soka nchini wakitoa maoni ya kuivusha klabu hiyo katika kipindi hiki cha mtikisiko wa kiuchumi.

Baadhi ya viongozi waandamizi wa zamani wa soka nchini, wametaja mambo matatu ya kuivusha Yanga katika kipindi cha mpito.

Mambo matatu yaliyotajwa na vigogo hao ni utulivu kwa wanachama, kuitisha uchaguzi mkuu haraka na kupata viongozi bora.

Bundi ameendelea kulia ndani ya Yanga baada ya Sanga kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana kwa madai ya kutishiwa kuuawa.

Sanga anakuwa mjumbe wa saba wa Kamati ya Utendaji ya Yanga kujiuzulu akitanguliwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Ayoub Nyenzi, Hashimu Abdallah, Salum Mkemi na Omari Saidi.

Baada ya vigogo hao kujiuzulu, Yanga imebakiwa na wajumbe watatu kati ya 10 waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa klabu hiyo mwaka 2016 ambao ni Samwel Lukumay, Thobias Lingalangala na Siza Lyimo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu, Iddi Kipingu alisema kitakachoivusha Yanga kwenye kipindi cha mpito ni wanachama kuwa watulivu na klabu kuitisha uchaguzi haraka.

"Unajua Yanga wanadai tatizo ni fedha, lakini kwa mazingira yalivyo sasa hawawezi kupata fedha, zaidi wataendelea kulumbana tu, ili watoke huko wanachama wanatakiwa kutulia, lakini pia walioachiwa kuendesha timu waitishe uchaguzi wa haraka," alisema Kipingu.

Kipingu alionya uchaguzi utakaoitishwa unakiwa kupata viongozi bora wenye dhamira ya kuiletea Yanga mafanikio na alitoa rai kwa wanachama kuwa makini wakati wa kupiga kura.

"Suala la ukata la muda mfupi, mambo yatakapotulia na klabu kuwa na uongozi 'strong' fedha itakuja tu wapo watu wanataka kuwekeza Yanga lakini kwa migogoro iliyopo wanashindwa," alisema Kipingu.

Rais wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage alisema mgogoro unaoendelea Yanga hauleti taswira nzuri kwa mustakabali wa soka nchini.

Rage alidai kuwa mgogoro wa Yanga utamalizwa na Wanayanga kwa kuwa wanafahamu kiini cha tatizo na aliwataka wanachama kutulia kutafuta ufumbuzi ili kuleta amani kwa kuwa klabu hiyo ikiwa katika matatizo Simba itakosa mshindani.

Mwenyekiti wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT) sasa TFF, Muhidin Ndolanga alisema Yanga inatakiwa kujipanga upya baada ya kufanya tathimini ya mgogoro ulioikumba klabu hiyo kongwe nchini.

“Alichofanya (Clement Sanga) ni sawa, lakini jambo la msingi ili kuivusha Yanga katika kipindi cha mpito ni kuitisha uchaguzi wa haraka kupata viongozi wapya wenye mtazamo chanya, kama watachelewa hata hao wachezaji watawakosa,” alisema Ndolanga.

Katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Sanga, alisema amemua kujiweka kando kwa kuwa tangu Yanga ilipopata mtikisiko wa kiuchumi, amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa yeye na familia yake.

"Nimelitazama kwa jicho la mbali zaidi. Imefika hatua mtu anazungumza bila kificho kuhamasisha watu waje nyumbani kwangu wakiwa na mapanga, majembe na mashoka utadhani Sanga ana shamba wanakuja kunisaidia kulima.

“Katika hali ya kushangaza, vitisho na taarifa hizi zimekuwa zikitolewa hadi kwenye magrupu ya mitandao ya kijamii ambayo mimi mwenyewe nipo, lakini sioni watu wakikemea hadi napata hisia kwamba pengine kuna watu wapo nyuma ya hili,” alisema Sanga.

Kigogo huyo alisema kutokana na klabu kutokuwa na viongozi wa juu kwa sasa, jukumu la kuiongoza linabaki mikononi mwa Baraza la Wadhamini.

Akizungumzia uvumi unaoenea kwenye mitandao ya kijamii viongozi wamefanya ubadhirifu wa fedha za klabu, alisema taarifa hizo zina lengo la kuwachafua.

“Ukweli lazima usemwe, mwenyekiti wetu aliyejiuzulu ndugu Yusuf Manji alikuwa akitoa kiasi kikubwa cha fedha kuendesha shughuli za klabu kiasi cha Sh1.5 bilioni kwa mwaka. Baada ya kujiuzulu tumekuwa kukiendesha klabu huku tukiwa hatuna vyanzo vingi vya mapato.

“Tunatumia zaidi ya Sh125 milioni kama bajeti ya mishahara kwa mwezi na bado kuna fedha tumekuwa tukikatwa na wizara ya ardhi, pia tumekuwa tukilipa madeni ya kesi mbalimbali ambazo klabu imeshindwa mahakamani," alifafanua Sanga.

Katika hatua nyingine, Sanga alidai hadi wakati anajiuzulu wadhifa wake, hakuwa amepokea barua rasmi ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Charles Mkwasa

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →