Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi katika klabu hiyo.
Sanga ametangaza uamuzi huo leo mbele ya waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika katika hotel ya Protea jijini Dar es salaam.
Sanga amesema amelazimika kujiuzulu akihofia usalama wake baada ya kupata taarifa juu ya uwepo wa watu wanaotaka kumvamia nyumbani kwake wakiwa na lengo la kumdhuru.
Sanga amekuwa kiongozi wa saba kuachia ngazi Yanga.
Bodi ya wadhamini ya Yanga italazimika kuteua uongozi wa mpito kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi wa dharura kujaza nafasi zilizowazi.
Kwa sasa Yanga haina watendaji wakuu baada ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wote kujiuzulu.
Lakini pia kuna wajumbe watano kutoka Kamati ya Utendaji na Kamati ya Mashindano ambao pia wamejiuzulu

ADVERTISE HERE