Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amethibitisha kuwa ni kweli amejiuzulu nafasi yake ya uongozi kutokana na matatizo ya kiafya.
Mkwasa amesema anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
"Ni kweli nilimuandikia barua Makamu Mwenyekiti kumueleza uamuzi wangu wa kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya yanayonikabili," Mkwasa ameiambia EFM.
Mkwasa amesema baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari alishauriwa apumzike wakati akisubiri kufanyiwa upasuaji mdogo.
Katika hali ya kushangaza Mkwasa amesema alianza kuugua maradhi hayo sambamba na Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten .
Mkwasa amesema ni yeye aliyemsaidia Ten baada ya kuanza kuugua ghafla wakiwa ofisini kabla nae maradhi kumkumba siku chache baadae.

ADVERTISE HERE