Uongozi wa timu ya Yanga umesema bado haujapokea barua rasmi ya kurejea kwa aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo Yusuph Manji aliyejiuzulu mwenzi uliopita baada ya kushauriwa na daktari wake.
Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kuwa mpaka sasa hawana taarifa rasmi ya kurejea kwa Manji na pindi watakapopata barua rasmi wataweka wazi.
Klabu ya Yanga kwa sasa ipo katika harakati za usajili wa wachezaji wapya pamoja na kuwaongezea mikataba wachezaji wao muhimu ambao mikataba yao inaelekea ukingoni.
Licha ya kwamba hajarejea rasmi ofisini lakini inadaiwa Manji ameiongezea Yanga fungu la usajili lilanowezesha klabu kusajili wachezaji wapya sambamba na kuongeza mikataba ya wachezaji wanaotakiwa kubaki klabuni.
Aidha Mkwassa amesema timu itakapomaliza zoezi la usajili itaweka hadharani kikosi kamili pamoja na kutaja majina ya wachezaji wanaoachwa.

ADVERTISE HERE