Dirisha la usajili litafungwa rasmi Alhamisi ijayo Julai 26 2018 saa 5.59 usiku, zimesalia siku tano tu.
Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji sita ambao ni Mohammed Issa 'Banka', Feisal Salim 'Fei Toto', Jaffar Mohammed, Deus Kaseke, Mrisho Ngassa na Heritier Makambo.
Yanga bado inahitaji kufanya maboresho kwenye safu yake ya ulinzi pamoja na ushambuliaji.
Kocha Mwinyi Zahera alipendekeza kusajiliwa wachezaji wengine watatu wa kigeni, wawili wakiwa washambuliaji, mmoja kiungo ambaye pia anaweza kucheza nafasi ya beki ya kati.
Licha ya kukabiliwa na changamoto za kiuchumi, juhudi kubwa zimekuwa zikifanywa na wadau mbalimbali wa Yanga kuhakikisha wachezaji wote waliopendekezwa na benchi la ufundi wanasajiliwa.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinabainisha leo Zahera atakutana na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Hussein Nyika.
Juzi Yanga iliporejea kutoka nchini Kenya, Zahera alisisitiza umuhimu wa timu hiyo kusajili wachezaji wapya .

ADVERTISE HERE