Kwa hivi vipigo vya 'mbwa koko' viongozi mjitafakari

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
19 Jul 2018
Kwa hivi vipigo vya 'mbwa koko' viongozi mjitafakari
kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia kimeendelea kudhihirisha umuhimu wa timu hiyo kufanya mabadiliko ili kujenga timu imara.

Viongozi wa Yanga hawawezi kukwepa lawama za mashabiki kwa mwenendo mbovu wa timu yao. Ingefaa huko waliko wajitathmini kama wanafaa kuendelea kukalia nafasi zao.

Yanga iliyocheza na Gor Mahia ni ileile iliyomaliza msimu kwa kufungwa mabao 3-1 na Azam FC lakini pia ndio ileile iliyokwenda kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.

Hakukuonekana mabadiliko yoyote kwa kikosi hicho kinachonolewa na Mcongo Mwinyi Zahera ambaye alikuwa jukwaani kushuhudia timu yake ikidhalilishwa ugenini.

Zahera bado hajapata kibali cha kumuwezesha kuiongoza Yanga kwenye michuano ya CAF.

Viongozi wa Yanga walitoa taarifa kuwa walituma majina ya wachezaji watatu waliowasajili CAF lakini wachezaji hao hawamo kwenye kikosi kwa kuwa bado hawajaidhinishwa na CAF.

Lakini Gor Mahia wachezaji wake iliyowasajili mwanzoni mwa mwezi huu wameweza kuidhinishwa na CAF kuwa sehemu ya kikosi cha Gor Mahia na wamecheza jana.

Licha ya uongozi wa Yanga kujitoa kwenye michuano ya kombe la Kagame wakitoa sababu ya wachezaji kuchoka lakini pia imekuwa na karibu mwezi mmoja wa kujiandaa na mchezo huo.

Yanga inahitaji mabadiliko makubwa kuanzia uongozi na pengine wachezaji.

Kwa sasa Yanga inatambulika kwa jezi zake pekee na sio ubora wa kikosi chake. Bila ya kuwa na wachezaji wenye viwango bora hakutakuwa na muujiza.

Yanga inapaswa kutumia ipasavyo dirisha la usajili wakati huu kuimarisha kikosi chake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’