Jiandae, uzi wa Yanga unakuja mikononi mwako karibuni

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
8 Aug 2017
Jiandae, uzi wa Yanga unakuja mikononi mwako karibuni
Moja ya mapinduzi makubwa ambayo klabu ya Yanga imekusudia kufanya msimu huu ni kunufaika na brand yake ambapo sasa bidhaa mbalimbali za Yanga zikiwemo jezi original zitaanza kupatikana kwa ajili ya mashabiki.

Huo ni mpango mzuri ambao utawezesha klabu kupunguza utegemezi kwani itaweza kuingiza mapato ya kutosha kutokana vyanzo vipya vya mapato.

Tumetaarifiwa jezi 'Original' za Yanga zitaanza kupatikani kwa bei rafiki siku chache zijazo.

Zitapatikana kwenye maduka maalumu ambayo yatawekwa hadharani na uongozi pindi mipango itakapokamilika.

Pia jezi hizo zitapatikana uwanjani katika michezo ambayo Yanga itakuwa inacheza.

Jezi ya Yanga ina ubora wa hali ya juu, imetengenezwa na kampuni ya Joma, kampuni maarufu inayotengeneza vifaa vya michezo duniani.

Hii itakuwa fursa nzuri kwa wewe shabiki wa Yanga kupendeza na uzi halisi wenye kiwango cha hali ya juu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’