Tangu mapema jana viongozi wa Simba walikuwa wakihaha kukamilisha usajili wa beki aliyemaliza mkataba na klabu ya Yanga Kelvin Yondani.
Jana viongozi hao walifanya kikao na Yondani ambapo leo inadaiwa ilikuwa akutanishwe na Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mo Dewji kumalizana nae fedha za usajili.
Hata hivyo kama kilichotokea kwa Fei Toto, mabosi wa usajili wa Yanga wameuwahi mchakato huo na kufanikiwa kumnyakua Yondani kabla hajatua kwa Mo Dewji.
Taarifa za uhakika ni kwamba leo Yondani anatarajiwa kusaini mkataba wa kuendelea kubaki Yanga.
Inaelezwa maridhiano yaliyofikiwa jana kati ya Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Mpito Abbasi Tarimba yamekuwa na faida kwani huenda hata Kessy nae atasaini mkataba mpya kuendelea kubaki Jangwani.

ADVERTISE HERE