Yanga matumaini kibao Kenya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
18 Jul 2018
Yanga matumaini kibao Kenya
Licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake waandamizi Kelvin Yondani na Hassani Kessy, wachezaji wa Yanga wamesema hawatakuwa tayari kupoteza mchezo wao wa leo dhidi ya Gor Mahia

Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa Yanga kwani matokeo ya ushindi yatawaweka katika nafasi nzuri mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania kabla ya mchezo wa marudiano baina ya timu hizo baada ya siku 10 jijini Dar es salaam.

Timu zote zinawania moja ya nafasi mbili za juu katika kundi ili kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho.

Kwa kutinga robo fainali, CAF itatoa kitita cha zaidi ya Mil 800 kwa timu zitakazofika hatua hiyo.

Yanga iliyoweka kambi Hoteli ya The Luke, jana jioni ilifanya mazoezi katika uwanja wa Moi Kasarani. Uwanja huo ndio utakaotumika kwenye mchezo wa leo.

Kocha Zahera amewatoa hofu mashabiki wa Yanga kuwa kikosi chake kiko kamili kuchuana na Gor Mahia licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake wazoefu.

“Nimeongea vizuri na wachezaji niliokuwa nao ingawa kukosekana kwa baadhi ya wazoefu inaweza kutuweka katika mazingira magumu, lakini hamna shida tumejipanga vizuri,” alisema.

Zahera akiizungumzia Gor Mahia, Zahera amesema timu hiyo inaundwa na wachezaji wengi wazoefu ambao aliwaona katika mashindano ya Sport Pesa na Kombe la Kagame yaliyomalizika Julai 13 jijini Dar es Salaam.

Lakini amesema Yanga inao uwezo wa kuifunga Gor Mahia baada ya kubaini kuwa na makosa mengi hasa kwenye safu yake ya ulinzi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →