Gor Mahia vs Yanga lolote linaweza kutokea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jul 2018
Gor Mahia vs Yanga lolote linaweza kutokea
Kesho saa moja jioni Yanga inashuka kwenye uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi kuikabili Gor Mahia katika mchezo wa tatu kombe la Shirikisho, kundi D.

Mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa Yanga kutokana na uimara wa kikosi cha Gor Mahia.

Wachezaji wa Gor Mahia wamekuwa pamoja kwa muda mrefu, wana mwendelezo mzuri wa kiwango chao.


Walikuja jijini Dar es salaam kushiriki michuano ya kombe la Kagame na wakafanikiwa kumaliza nafasi ya tatu.

Timu hiyo pia inaongoza ligi kuu ya Kenya ambayo kalenda yake inapishana na kalenda ya Tanzania.

Hali ni tofauti kwa Yanga. Baada ya kumalizika kwa michuano ya Sportpesa Super Cup,wachezaji wa timu hiyo walipewa mapumziko.

Yanga imefanya mazoezi kwa takribani wiki tatu kabla ya mchezo huo.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Mcongo Mwinyi Zahera, kitakuwa kinacheza mchezo wake wa kwanza wa kimashindano tangu kilipoanza kujifua mwishoni mwa mwezi Juni.

Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu kupata matokeo nchini Kenya, ingawa amekiri mchezo hautakuwa mwepesi.

Yanga haitakuwa na mpira kwa muda mwingi

Gor Mahia inafahamika kwa kucheza mchezo wa kumiliki mpira kwa muda mwingi 'possesion football' hivyo ni wazi mapambano makali yatakuwa kwenye sehemu ya kiungo.

Zahera atalazimika kujaza viungo wengi katikati ili kuweza kudhibiti madhara ya viungo wa Gor Mahia watakaongozwa na Francis Kahata.

Walipokuja kwenye michuano ya kombe la Kagame, Gor Mahia walifungwa na Azam Fc mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali ambao ulipigwa kwa dakika 120.

Azam walifanikiwa kuwadhibiti Gor Mahia kwa kuwa hawakuwaruhusu wacheze mpira katika maeneo ya hatari.

Na mara nyingi timu inayokaa na mpira kwa muda mwingi, wakati wowote inaweza kufungwa kupitia mashambulizi ya kushitukiza.

Yanga ina watu wenye kasi kama Geofrey Mwashiuya, Emanuel Martin na Juma Mahadhi. Wachezaji hawa wanaweza kuwapa wakati mgumu walinzi wa Gor Mahia.

Timu zote zitaingia kwenye mchezo huo zikiwa na lengo la kupata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga robo fainali.

Gor Mahia itakuwa na faida ya sapoti kubwa ya mashabiki wake kwa kuwa itakuwa inacheza uwanja wa nyumbani.

Lakini haimaanishi kwamba watapata urahisi wa kuifunga Yanga. Kila mmoja atalazimika kufanya kazi ya ziada ili kuweza kuibuka na ushindi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
9h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
13h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
14h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
14h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’