Winga wa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Bara Mrisho Ngassa ameishukuru klabu ya Ndanda FC kwa ushirikiano waliompa katika kipindi cha miezi sita alichoitumikia.
Ngassa aliitumikia Ndanda FC kwenye duru ya pili ya ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita akijiunga nao akitokea klabu ya Mbeya City aliyoitumikia kwenye duru ya kwanza.
"Kila Jambo ni mungu, nashukuru klabu ya Ndanda kwa mazuri walionionyesha. Hakika nimejifunza vingi kwenu nimecheza kwa kuona kama nipo nyumbani moyo wangu ulikuwa na amani," amesema Ngassa.
Ngassa alitoa kauli hiyo jana muda mfupi baada ya kutambulishwa kuwa mchezaji halali wa Yanga.
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye kasi alikuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia Ndanda FC kubaki ligi kuu msimu ujao.
Ameondoka katika klabu hiyo akiwa mchezaji huru sambamba na wachezaji wengine sita walioiacha Ndanda FC na kujiunga na timu nyingine.

ADVERTISE HERE