Yanayojiri Urusi : Shamrashamra za kombe la dunia zafika tamati leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2018
Yanayojiri Urusi : Shamrashamra za kombe la dunia zafika tamati leo
Michuano ya kombe la dunia iliyoanza Urusi Juni 14 2018 inafikia tamati leo kwa kupigwa mchezo wa fainali kati ya Ufaransa dhidi ya Croatia.

Michuano ya mwaka huu imekuwa na msisimko wa aina yake ambapo ilishuhudia baadhi ya vigogo wakiondoshwa mapema kwenye michuano hiyo.

Ujerumani mabingwa watetezi walishindwa kupenya hatua ya makundi huku Argentina iliyocheza fainali mwaka 2014 ikiondoshwa katika hatua ya 16 bora.

Ureno iliyokuwa inaongozwa na mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo nayo iliangukia pua katika hatua ya 16 bora.

Wenyeji wa michuano hiyo Urusi ambao wengi waliwaona kama vibonde, waliiduwaza dunia baada ya kuwaondosha vigogo wengine Hispania katika hatua ya 16 bora na kufanikiwa kutinga robo fainali.

Brazil iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo nayo ikaondoshwa na Ubelgiji katika hatua ya robo fainali.

Mashindano ya mwaka huu hayakuwa mazuri kwa upande wa Afrika kwani timu zake zote ziliishia kwenye hatua ya makundi huku Senegal ikiondoshwa kwa sheria ya kadi za njano baada ya kufanana takwimu na Japani.

Mchezo wa fainali unazikutanisha timu zenye sifa tofauti. Ufaransa itakuwa inajaribu kushinda kombe la dunia kwa mara ya pili ikifanya hivyo mara ya kwanza mwaka 1998.

Croatia haijawahi kushinda taji hilo, aidha hii ni mara yao ya kwanza kutinga fainali.

Takwimu za miaka ya nyuma zinaibeba zaidi Ufaransa kuelekea mchezo huo wa fainali utakaopigwa leo Jumapili, Julai 15 saa 12 jioni.

Ufaransa haijawahi kufungwa na Croatia katika mashindano yoyote ambayo timu hizo zimekutana.

Ufaransa na Croatia zimekutana mara tano, Ufaransa imeshinda michezo mitatu wakati miwili zilitoka sare.

Mwaka 1998 timu hizo zilikutana kwenye nusu fainali ya michuano hiyo na Ufaransa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na ikaenda kushinda taji hilo kwa kuwabamiza Brazil mabao 3-0.

Croatia imetinga fainali kwa michezo yake mitatu ya hatua ya 16 bora, robo fainali na nusu fainali yote kwenda muda wa ziada.

Kwa maana nyingine, timu hiyo imecheza zaidi ya dakika 360 ukianzia hatua ya 16 bora mpaka kufika fainali wakati Ufaransa imetumia dakika 270 pekee kutinga fainali.

Ufaransa inaweza kutwaa taji hilo kwa kuibuka na ushindi katika muda wa dakika 90 lakini watakuwa hatarini kufungwa kama wataruhusu kwenda muda wa ziada.

Croatia imeonyesha umahiri wa kushinda michezo kwenye muda wa ziada na hata kwenye matuta hasa inapotokea nyuma.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’