Yaliyoikuta Simba kwa Buswita, yataikuta Singida United kwa Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2018
Yaliyoikuta Simba kwa Buswita, yataikuta Singida United kwa Fei Toto
Viongozi wa timu ya JKU wamethibitisha kuwa Singida United haikuwahi kuwasiliana nao kabla ya kutangaza wamemsajili Feisal Salum 'Fei Toto'.

Fei Toto alikuwa na mkataba wa miaka miwili na JKU hivyo kwa maeleze ya viongozi wa klabu hiyo, ni wazi Singida United walifanya makosa kufanya mazungumzo, kisha kumsajili mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine.

Kanuni za usajili za FIFA ziko wazi, timu A inaruhusiwa kufanya mazungumzo na mchezaji bila kuwasiliana na timu B inayommiliki mchezaji huyo kama mkataba wake ni chini ya miezi sita.

Lakini si hivyo kwa mchezaji mwenye mkataba wa zaidi ya miezi sita. Kwa tukio hilo, JKU wanaweza kwenda kushitaki FIFA na Singida United ikaadhibiwa.

Madai pekee ambayo Singida United wanastahili kulipwa ni fedha walizompa Feisal. Wanaweza hata kwenda Mahakamani kushitaki ili warudishiwe fedha zao.

Naamini viongozi wa Yanga watamalizana na Singida United kwa kuwarudishia fedha walizompa Fei Toto.

Tukio walilofanya Singida United halina tofauti na tukio walilofanya Simba kwa Pius Buswita msimu uliopita.

Simba walimfuata Buswita na kumpa Mil 10 kisha wakamsainisha mkataba bila ya kuihusisha Mbao FC ambayo ilikuwa ikimmiliki Buswita kihalali.

Yanga ikafanya hiki ilichofanya kwa Feisal, kwa kuwasiliana na viongozi wa Mbao Fc kisha kumsajili Buswita kihalali.

TFF ilimfungia Buswita 'kimakosa', maamuzi waliyoyafikia baadae ndio yalikuwa maamuzi sahihi.

TFF ilimtaka Buswita alipe Mil 10 alizochukua Simba ndio aruhusiwe kuitumikia Yanga. Fedha hiyo ililipwa na Buswita akawa mchezaji halali wa Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’