Yondani, Kessy hatihati kuikosa Gor Mahia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2018
Yondani, Kessy hatihati kuikosa Gor Mahia
Wakati Yanga ikitarajiwa kuondoka kesho Jumatatu kuelekea Nairobi Kenya kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumatano Julai 18, walinzi Hassani Kessy na Kelvin Yondani wanaweza kukosa mchezo huo.

Licha ya kumalizana na wachezaji wote waliokuwa wakiidai Yanga madeni ya nyuma, inaelezwa Kessy na Yondani hawajafanya mazoezi na kikosi hicho wakisubiri kukamilishwa kwa madai yao ya fedha za usajili kwa ajili ya kandarasi mpya.



Yanga iliweza kuwarejesha wachezaji wake wote kikosini baada ya kuwalipa madeni yao ya nyuma hata hivyo inaelezwa wapo baadhi ambao bado hawajalipwa fedha za usajili kwa ajili ya kandarasi mpya.

Mlinda lango Benno Kakolanya, walinzi Juma Abdul na Andrew Vicent waliweza kufanya mazoezi kwa siku kadhaa baada ya kumalizana na uongozi wa Yanga lakini kuna taarifa nao wana madai ya fedha za kandarasi mpya.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema wamekuwa wakifanya mazungumzo na mchezaji mmoja mmoja, amesema kila mwenye madai yake atalipwa.

Wakati hayo yakiendelea, Yanga inaendelea kusajili wachezaji wapya ambapo jana imewatambulisha winga Mrisho Ngassa na Deus Kaseke.

Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Ndanda FC wakati Kaseke amerejea na kusaini kandarasi ya miaka miwili akitokea klabu ya Singida United.'

Mpaka sasa Yanga imetambulisha usajili wa wachezaji watano ambao ni Mohammed Issa 'Banka', Jaffar Mohammed, Fiesal Salum 'Fei Toto', Mrisho Ngassa na Deus Kaseke.

Nyika amesema huenda akatambulisha usajili wa mchezaji mwingine kabla Yanga haijatimka kwenda Kenya. Mcongo Heritier Makambo anatajwa kuwa mchezaji huyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’