Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetoa maamuzi juu ya maombi ya dhamana ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji baada ya shauri hilo kuahirishwa Agosti 04.
Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Isaya ametupilia mbali maombi ya dhamana ya Manji baada ya kukubaliana na pingamizi la upande wa Serikali.
Manji alipeleka maombi hayo katika mahakama hiyo kupinga hati iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuzuia dhamana dhidi yake.
Manji na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe, plate number mbili za magari ya serikali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

ADVERTISE HERE