Azam FC imeichapa Simba mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali na kufanikiwa kuhifadhi taji la Kagame kwa mara ya pili.
Ilitwaa taji hilo mara ya kwanza mwaka 2015.
Shabani Idi Chilunda na Aggrey Morris ndio waliopeleka kilio msimbazi, wakati bao pekee la Simba likifungwa na Meddie Kagere.
Mlinda lango wa Azam FC Razak Abarola aliikosesha timu yake ushindi ulionona zaidi baada ya kukosa mkwaju wa penati.
Azam FC ilikuwa timu bora kwenye mashindano hayo ambayo Yanga ilijitoa ili kujikita na maandalizi ya michuano ya kombe la Shirikisho.
Gor Mahia wapinzani wa Yanga kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Jumatano ijayo jijini Nairobi, wamemaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga JKU kwa mabao 2-0.
Gor Mahia imeonyesha kiwango cha kawaida sana kwenye michuano hiyo, Yanga ina nafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Jumatano.
Aidha, mapumziko waliyopewa wachezaji Yanga huenda yakainufaisha timu hiyo katika mchezo wa Jumatano tofauti na wapinzani wao ambao watakuwa na siku tatu za kupumzika kabla ya mchezo huo.

ADVERTISE HERE