Nyika aunga mkono usajili wa wachezaji 10 wa kigeni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jul 2018
Nyika aunga mkono usajili wa wachezaji 10 wa kigeni
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika ameunga mkono kuongezwa kwa idadi ya usajili wa wachezaji wa kigeni kutoka saba hadi kumi.

Nyika amesema uamuzi huo utakuwa na manufaa kwa vilabu lakini pia utatoa changamoto kwa wachezaji wazawa.

"Uamuzi huo tumeupokea kwa furaha kwani utakuwa na manufaa kwa vilabu. Lakini pia utawapa changamoto ya kuweza kuimarisha viwango vya wachezaji wazawa," Nyika ameiambia EFM.

Jana Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) ilipitisha kanuni za kuruhusu usajili wa idadi ya Wachezaji 10 wa Kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao.

TFF imesema wachezaji hao wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja.

Yanga ina wachezaji watano wa kigeni ambao ni Youthe Rostand, Papi Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Heritier Makambo.

Baada ya mabadiliko ya kanuni, mabingwa hao wa kihistoria Tanzanoia Bara wanaweza kusajili wachezaji wengine watano wa kigeni.

Yanga inaendelea kuwafanyia majaribio wachezaji watatu, wawili kutoka Nigeria na mmoja kiungo kutoka Afrika Kusini.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’